Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (S) yametoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, yakisema kuwa endapo mashambulizi dhidi ya kusini mwa Lebanon yataendelea, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatoa jibu kali kupitia vikosi vyake vya ulinzi.
Katika taarifa yake, Makao Makuu hayo yalisema kuwa jeshi la Israel limekiuka makubaliano ya usitishaji mapigano mara 84 katika kipindi cha siku mbili zilizopita, licha ya kutangazwa kwa kumalizika kwa vita na Rais wa Marekani.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa jeshi la Israel linaendelea kufanya ukiukaji wa makubaliano hayo pamoja na mashambulizi yanayosababisha vifo vya raia wa Lebanon.
Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (S) yamesisitiza kuwa ikiwa Israel haitasitisha mashambulizi yake dhidi ya kusini mwa Lebanon, italazimika kukabiliana na jibu kali kutoka kwa Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Your Comment